Unahisi kama hauna usalama katika uhusiano wako?
Una maswali?
Ungependa kuongea na mtu?
Kuna mtu ambae atakusikiliza.

Usinyamaze. Kuna msaidizi ambae anaweza kusaidiana nawe kupata kutatua.
Kwa maelezo zaidi, piga simu bila kujulikana kwa msaidizi katika lugha yako.

tuite!

Nini kinaweza kutokea?

  • Mwenzio anachunguza unachofanya, nguo unazovaa, simu yako ya mkononi, vyombo vya habari vya kijamii, mawasiliano yako...
  • Huwezi kuonana au kuzungumza na familia yako au marafiki wako wakati unapotaka, unajisikia kama uko pekee yako.
  • JHuwezi kuondoka ama kuja nyumbani wakati unapotaka.
  • Huwezi kufanya kazi, kusoma lugha ama kufuata masomo unayotaka.
  • Hakuna anayekusikiliza na huwezi kufanya maamuzi kuhusu maswala ambayo yanakuhusu wewe ama watoto wako.
  • Mwenzio anatisha kuchukua karatasi zako na watoto wako
  • Huwezi kutumia kadi lako la benki ama pesa zako mwenyewe unavyotaka
  • Huwezi kuwa na uhusiano na mtu yeyote unavyotaka.
  • Unapigwa.
  • Unalazimishwa kufanya mapenzi.
  • Unaguswa bila ruhusa yako na huwezi kuenda popote kutafuta usaidizi.
  • Huwezi kupanga uzazi.
  • Unahisi kama unaumizwa.
  • Haujiamini tena.
  • Unahisi kama unaaibishwa.
  • Unafungwa ama unafungiwa.
  • (..)

Haya ni mifano ya unyanyasaji wa kimwili, kijinsia, kifedha, kisaikolojia na kihisia. Mara nyingi una hofu na afya yako na ya watoto wako yanaharibika. Unahitaji mtu ambae anakusikiliza.

Unaweza kuboresha hali yako kwa njia tofauti:

  • Unaweza kutafuta mawaidha, unaweza kumpigia mtu fulani simu, unaweza kwenda mahali fulani, ...
  • Una haki ya kutafuta usaidizi unaokufaa wakati unaotaka.
  • Hakuna anaeweza kukulazimisha kufuata hatua usizotaka kufuata.

Kuna watu ambao wanaweza kukusikiliza na kusaidiana nawe kutafuta suluhisho ama usaidizi. Unaweza kuwasiliana nao bila kujulikana kupitia:

Pia kwa maswali kuhusu watoto wako, unaweza kupiga simu kwa nambari ifuatayo. Una haki ya kuona watoto wako. Hakuna mtu anayeweza kukunyima haki hii.

Unafaa kujua nini unaweza kufanya

OIli kufanya uamuzi kuhusu hali yako, ni muhimu kujua chaguo zako zote na haki yako. Msaidizi wako katika lugha yako anaweza kukupa maelezo na usaidizi kuhusu mawezekano yote na suluhisho kupitia njia ya simu bila kujulikana.

tuite!

Unaweza pia kutafuta habari na maelezo zaidi mwenyewe. Huduma muhimu zaidi na maelezo katika kiholanzi/kifaransa yanapatikana hapa chini.

Unaweza kufanya nini?

Unaweza kwenda wapi?

Mtu anayekusikiliza kwa lugha yako.

Usisite kuwasiliana bila kujulikana na mtu anayeweza kukusikiliza katika lugha yako. Hauko pekee yako, kuna mtu ambae yuko tayari kukusikiliza.

tuite!

Kwa msaada ya kijamii na maelezo ya jumla

Piga simu au tuma barua pepe kwa 1712 kwa maswali kuhusu unyanyasaji wa kinyumbani. Kupiga simu kwa 1712 ni bure na haionyeswi kwenye malipo. maelezo zaidi yanapatikana katika www.1712.be

Piga simu, tuma barua pepe au tembelea Kituo cha Kazi la Ustawi (CAW). CAW itasikia hadithi yako na itatafuta pamoja nawe jinsi inavyoweza kukusaidia zaidi. Mawasiliano na CAW ni bure na inaweza kufanyika bila kujulikana. Vituo vya CAW vinapatikana Flanders nzima. Maelezo zaidi yanapatikana kwa www.caw.be au kwenye nambari la simu 0800 13 500.

Kwa maswali kuhusu usaidizi, msaada wa kisaikolojia, ushauri wa kisheria na kadhalika, unaweza kupiga simu kupitia nambari 0800 30 030 (Kifaransa) au kupitia www.ecouteviolencesconjugales.be

Kituo cha Umma cha Ustawi wa Jamii (OCMW). Kila munispaa au mji una OCMW yake ambayo hutoa huduma mbalimbali. Usaidizi wa kijamii unaweza kupatikana kwenye kituo cha OCMW katika manispaa au jiji lako. Maelezo zaidi yanapatikana kwa www.belgium.be/nl/familie/sociale_steun/ocmw

Kwa ajili ya mapokezi

Maelezo ya mawasiliano ya vituo mbalimbali vya wakimbizi na vituo vya upokezi wa wanawake yanapatikana kupitia nambari la simu 1712, Jumatatu hadi Jumamosi kati ya saa 9.00 asubuhi na saa 17.00 jioni au kupitia vituo vya CAW. Maelezo zaidi yanapatikana katikawww.caw.be Au kupitia www.ecouteviolencesconjugales.be\maisons.php 0800 30 030

Maelezo ya kisheria

Kwa ushauri wa kisheria na maelezo ya kisheria unaweza kuwasiliana na mwanasheria. Ushauri wa kwanza ni bure. Ikiwa huna uwezo wa kulipia msaada huu, una haki ya ushauri wa bure kupitia mwanasheria wa pro-deo. Maelezo zaidi kuhusu msaada wa kisheria na wanasheria yanapatikana katika

Maelezo kuhusu hali yako ya makazi

Waathiriwa wa unyanyasaji wa kimapenzi wanapashwa kulindwa, hata ikiwa wamekuja Ubelgiji ili kuungana na familia. Angalia ni hatua gani wewe mwenyewe au mwanasheria wa maswala ya uhamiaji anaye kusaidia mnaweza kuchukua ili kuweza kukukinga na matokeo ya hatua hizi kwa uwezo wako wa kuendelea kuishi Ubelgiji. Maelezo zaidi yanapatikana katika www.cire.be .

Kwa maelezo zaidi kuhusu wanasheria, nyaraka za makazi, sheria la uhamiaji na sheria ya kimataifa ya familia (kwa mfano ikiwa wewe au mpenzi wako ana paspoti la kigeni au hana visa ya kudumu ya makazi) nenda kwa www.integratie-inburgering.be/juridische-dienstverlening au piga simu kwa 02 205 00 55. Maelezo zaidi yanapatikana katika www.agii.be/thema/vreemdelingenrecht-internationaal-privaatrecht au www.progresslaw.net

Polisi na msaada wa matibabu

Kwa kila tukio, nenda kwa daktari au hospitali, uliza matokeo ya matibabu na mweleze daktari akuwekee matokeo haya. Daktari wako ana maelekezo maalum ya kukabiliana na waathirika wa unyanyasaji.

Maelezo zaidi kuhusu polisi katika eneo lako yanapatikana katika www.politie.be/nl

Ikiwa unahitaji msaada wa haraka kwa mfano katika hali inayohatarisha maisha, piga simu kwa polisi kupitia 101. Polisi wanalazimika kukusaidia. Ikiwa unahitaji matibabu ya haraka, piga simu mara moja kwa namba ya dharura ya 112

Kwa maelezo ya jumla

Maelezo kuhusu unyanyasaji wa kimapenzi:

Unyanyasaji wa kimapenzi unaadhibika

Ikiwa (baadaye) unataka kufanya malalamishi kwa polisi, fuata vidokezi hivi

  • Beba vyeti vya matibabu kutoka kwa daktari au hospitali.
  • Chukua kopi au picha ya vyeti na kadhalika. Weka vyeti asili kwa makini au uliza daktari wako aziweke kwa niaba yako.
  • Soma kwa makini kabla ya kuweka sahihi. Chukua mda wako kusoma na ikiwa kuna kifungo ambacho hakieleweki, uliza kibadilishwe
  • Omba nakala ya malalamishi yako, nambari ya ripoti rasmi na jina la mtu ambae alisajili malalamishi yako. Unaweza kutumia mkusanyiko huu wa data baadaye ikiwa utaamua kufungua malalamishi, kutengana au kuishi pekee yako.

Ikiwa unatafuta makazi yenye usalama:

  • Weka makaratasi muhimu tayari (yako na ya watoto wako): vitambulisho, nambari ya faida ya watoto, ikiwa umeolewa: cheti cha ndoa na kopi yake, ikiwa mnaishi pamoja kisheria lakini hamjaoana: vyeti vya ununuaji wa vyombo au mali uliyonunua mwenyewe au mliyonunua kwa pamoja (ankara, kauli za akaunti), vyeti vya matibabu ya majeraha kutokana na kupigwa.
  • Ikiwezekana: weka pesa kando ya kukodisha au kuweza kulipia usafiri kwa marafiki. Wajulishe mapema kwenda kwako
  • Weka mifuko midogo tayari yenye nguo yako na mali yako kwa jirani au mtu yeyote anaeaminika ikiwa utapaswa kuondoka kwa haraka.
  • Weka vitu vyako vya umuhimu na vyenye dhamana tayari
  • kiwa una gari la kibinafsi: weka ndani vitu ambavyo vinaweza kukusaidia kuhisi kama una usalama
  • Ikiwa kuna utengano, weka picha ya vyumba vyote nyumbani, vifaa vyote, samani...
  • Unapoondoka, weka sahihi ili kuondoa ushirika wa mpenzi wako kwenye akaunti zako za benki.
  • Omba shirika la posta liweke barua zako au zitumwe kwako mwenyewe. Shirika la posta halina ruhusa ya kupeana bure anwani yako.

www.vzwzijn.be/upload/docs/ZIJN_folder2_slachtoffervanpartnergeweld.pdf